Jicho La Tatu (Kifungu cha 4): Usichambue Uzoefu Wako Katika Maono

Rakims Spiritual
0

Jicho La Tatu: Sheria na Taratibu

Kifungu cha 4: Usichambue uzoefu wako wakati wa maono

Jicho la tatu ni nini? Rejea katika video zetu husika ndani ya playlist ya Jicho la Tatu ili kutambua maana, faida, hasara zake, ikiwa ni pamoja na mwongozo kamili wa awali.

Katika makala hii, tunaendelea na mwongozo kwa wale wanaoendelea na mazoezi. Hapo awali tuliwatambulisha na kuvielezea vifungu vitatu vya mwanzo. Leo tutaangalia kwa kina Kifungu cha Nne.

👁️ Sheria ya Nne: Kutokuchambua uzoefu wako. Wakati mwanafunzi akiendelea na mazoezi, hufikia hatua ya majaribu ambayo yatamtaka kuchambua (analyze) kile anachokiona kwa wakati huo.
Abstract mystical purple light representing the inner visions of the Third Eye.

Kumbukumbu ya Vifungu vya Awali

Sheria hii ya nne inakuja tu baada ya mwanafunzi kufuata kwa usahihi sheria zote tatu za awali, ambazo ni:

1. Kutokulazimisha: Kutokulazimisha wala kukariri katika zoezi lako; lengo kuu ni kuelewa tu kile unachokifanya.
2. Kuepuka Picha za Uongo: Kutokutengeneza picha au matarajio katika fikra zako kuhusu hatua zijazo zinazofuata.
3. Kuamini Uelewa: Kuamini na kukubali kile unachoanza kukielewa vema ndani ya roho yako.

Kifungu cha 4: Hatari ya Kuchambua Maono

Hivyo basi, mwanafunzi wa mazoezi haya ya kufungua Jicho la Tatu hufikia hatua ambayo itamjaribu kuchambua kile anachokiona.

Mfano: Wakati wa zoezi, inaweza kumtokea mwanga ghafla mbele ya macho yake ambayo ameyafumba. Hapo hapo, akili yake huanza kuisukuma nafsi na kujiuliza, "Hiki ni nini ninachokiona?"

Katika hatua hii, wanafunzi wengi hufanya kosa la kufumbua macho haraka na kumuuliza mwalimu. Kitendo hiki humtoa mwanafunzi katika zoezi zima na kumtaka aanze upya tangu mwanzo. Unapaswa kuelewa wazi kuwa hutakiwi kuchambua kinachotokea kwenye maono yako.

⚠️ Onyo Muhimu: Ukianza kutumia akili yako ya kawaida kuchambua na kujiuliza maswali juu ya kile unachokiona, huo ndio unakuwa mwanzo wa maono ya udanganyifu (illusions). Akili yako itaanza kukutengenezea picha za uongo badala ya kuona ukweli wa kiroho.

Nini Unachotakiwa Kufanya?

Mwanafunzi wa masomo haya tunamtaka aendelee kubaki katika uzoefu wake, haijalishi ni kitu gani kimetokea au kupita katika maono yake. Anachotakiwa kufanya ni kuendelea na zoezi bila kusita wala kukwama.

Hicho unachoendelea kukiona si kitu kipya; ni jambo lililopo mbele yako siku zote katika ulimwengu wa kiroho. Huwa ni sawa na mtu ambaye alikuwa amefunga macho yake maisha yake yote, na sasa anaanza kujifunza kutazama na kuelewa mazingira yake mapya. Jipe muda.

✨ Kwa mwanafunzi ambaye atafanikiwa kupita hatua hii bila kujiuliza maswali, basi moja kwa moja anakuwa amefuzu katika kukwepa ulaghai wa maono.

Hatua Inayofuata

Kifungu kitakachofuata ni Kinga ya Zoezi Hili. Nacho tutakichambua vema wakati wa kumalizia vifungu vingine na kuanza mazoezi rasmi.

Makala hii haikukatazi wewe kuendelea na mazoezi yako unayofanya kila siku na walimu waliokufundisha awali, bali huu ni mwongozo sahihi zaidi wa kukuwezesha kuelewa kwa kina zaidi ya vile ulivyotambua awali.

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)
Our website uses cookies to enhance your experience. Learn more
Accept
💬 Get Guidance