Jicho La Tatu (Kifungu 2 & 3): Usiunde Picha na Amini Uzoefu Wako

Rakims Spiritual
0

Jicho La Tatu: Sheria na Taratibu

Kifungu cha 2 & 3: Hakuna kuunda picha na kuamini uzoefu wako

Kifungu cha 2: Hakuna Kuunda Wala Kudhani Picha

Katika mwendelezo wa sheria na taratibu muhimu za kufungua Jicho la Tatu, Kifungu cha Pili kinabeba uzito mkubwa. Mtu mwenye nia ya kufungua ufahamu huu wa kiroho anapaswa kuepuka makosa yafuatayo kwa gharama yoyote:

Kutokuunda picha katika akili yake.
Kutokudhania (kuhisi/kubashiri) picha kwenye fikra zake.

Ikiwa unaendelea na mazoezi yako na ghafla ikatokea picha, mwangaza, nuru, au hata kiumbe cha kiroho kikaja kwenye maono yako—usikijali. Endelea na zoezi lako pekee. Usianze kuweweseka au kujaribu kufikiri kwa sababu tu umesikia kwamba "wenye kufanya mazoezi haya huona vitu fulani."

Abstract mystical light and smoke representing the formless visions of the Third Eye.

Hatari ya Kujitengenezea Maono (Illusions)

Ni marufuku kufikiria au kuchambua kile kinachotokea kwenye maono yako. Moja ya sababu kubwa ya kuzuia hili ni kulinda ukweli wa maono yako.

Chukulia mfano huu: Labda ukajiwa na "malaika" katika zoezi lako. Kama akili yako inaruhusiwa kuunda picha, hutajua kamwe kama huyo ni malaika wa kweli wa kiroho, au ni malaika aliyetengenezwa na akili yako mwenyewe (hallucination/illusion).

⚠️ Tatizo Lipo Wapi? Shida si kwamba hutaona—utaona vizuri tu. Shida inakuja kwenye ukweli wa kile ambacho hiyo roho itakuambia au kukuongoza. Je, ni roho kweli? Au ni akili yako mwenyewe ambayo mwisho wa siku itakuja kumpotosha na kukupoteza mbali?

Mifano Hai: Virtual Reality (VR) na Jicho la Tatu

Neno kuu katika meditation ya kawaida ni Kutulia. Neno kuu katika meditation ya Jicho la Tatu ni Uelewa. Unapaswa kuelewa tu kuwa unafanya zoezi, na usilewe (usipotee) kana kwamba wewe ni sehemu ya maono hayo.

🎮 Mfano wa Virtual Reality: Chukulia unacheza mchezo wa Virtual Reality (VR). Picha zinazoendelea muda huo ni Jicho la Tatu lipo wazi. Kadri unavyozidi kuingia ndani na kutulia, ndivyo unavyozidi kuona. Lakini, ukianza kushtuka, kupiga kelele, au kureact (kuchambua)—moja kwa moja mashine itazimwa. Ukireact kwenye Jicho la Tatu, maono hukatika papo hapo.

Kifungu cha 3: Amini Uzoefu Wako

Tunapoendelea na sheria ya tatu, tunakutana na msingi mwingine thabiti: Kuamini uzoefu wako katika zoezi zima la kufungua Jicho la Tatu. Hii ni moja kati ya sheria muhimu sana kati ya zile 9 za kufungua ufahamu huu.

Kama huna kitu cha kukiamini, basi pia haupaswi kuwa na kitu cha kukipinga kikikutokea. Kwa kuwa umezuiwa kutengeneza picha au fikra yoyote (Sheria ya 2), basi usipoteze muda wako kuhofia kuhusu kile unachokiona. Usijiulize, "Je, kweli naona hivi au ni mawazo yangu?"

Jinsi Maono Yanavyojitokeza

Amini uzoefu unaopitia. Jinsi unavyoendelea kufanya mazoezi haya kwa utulivu na kuondosha "pumba na mchele" kwenye akili yako, ndivyo uelewa wako wa utambuzi wa maono utazidi kufunguka. Kwako itakuja kuwa wepesi hata kuelewa mambo katika uhalisia wa ulimwengu wa kawaida.

🌫️ Asili ya Maono: Unatakiwa kuamini kuwa kile unachokiona ni maono ya kweli. Mara nyingi, maono haya huja kama "picha za moshi" (hazy shapes) zinazosubiria akili yako iziumbe. Sheria zinakataa wewe kuziumba! Acha ule moshi au mwanga ujifungue wenyewe bila wewe kuuchunguza au kuusaidia.

Hatua Inayofuata

Video na makala ijayo itachambua kwa kirefu sana Kifungu cha 4, ambacho kinakataza kuchambua yale yanayoendelea katika uzoefu wako. Pia tutaelezea jambo la muhimu zaidi katika zoezi hili ili kuhakikisha hukwami katika safari yako ya kiroho.

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)
Our website uses cookies to enhance your experience. Learn more
Accept
💬 Get Guidance