Hypnosis (Sanaa ya Fikra)
Gundua nguvu iliyofichwa ya akili yako ya ufahamu wa chini
Katika makala hii, nitakueleza kwa uchache kuhusu Hypnosis—nikiwa na maana ya sanaa ya kupangua, kubadili, na kuhama kutoka sehemu moja ya fikra kwenda nyingine.
Hypnosis ni hali ya kiakili inayohusisha umakini mkubwa na uvutivu wa maono (focused concentration) kwa kiwango cha juu sana. Wakati upo kwenye hali hii, unakuwa na ufahamu mdogo sana wa mazingira yanayokuzunguka, na akili yako inakuwa wazi kabisa kupokea maelekezo au mapendekezo (suggestions).
Faida za Hypnosis
Kila jambo kabla ya kulianza, ni vyema kujua faida zake. Kuhypnotize ubongo kuna faida zifuatazo kubwa:
- Kufikia Malengo Makuu: Inamsaidia muhusika kufikia yale aliyokuwa akiyaona hayawezekani katika uhalisia, na kumjengea ujasiri mkubwa.
- Kuondoa Msongo wa Mawazo: Inamsaidia muhusika kuondokana na stress, wasiwasi mkubwa, na hofu zilizojificha (phobias).
- Kupunguza Maumivu: Husaidia kuondoa au kupunguza maumivu makali mwilini, ikiwemo maumivu ya kansa, migraines (kuumwa kichwa upande mmoja), na kulegeza misuli.
- Kubadili Tabia: Hii ni faida kubwa zaidi. Husaidia sana kuacha tabia sugu kama uvutaji sigara, ulevi, kukosa usingizi (insomnia), wizi, na uoga wa kupindukia.
Nani Anafaa Kufanya Hypnosis?
Hypnosis inaweza kufanya kazi kwa karibu kila mtu, ingawa baadhi ya watu wanashawishika (susceptible) haraka zaidi kuliko wengine. Watoto na vijana mara nyingi ni wagombea wazuri sana kwa sababu wana akili zilizo wazi na imagination (fikra za picha) nzuri sana.
Muhimu: Ikiwa humuamini mtaalamu wako (hypnotherapist), au huamini kama hypnosis itafanya kazi kwako, haitefanya kazi. Hypnosis inafanya kazi tu ikiwa uko tayari (willing) kuruhusu ifanye kazi.
Tahadhari na Hatari Zake
Kama tunavyojua, hakuna chenye faida kisicho na kikwazo. Ingawa hatari hizi ni nadra sana, yaweza kukutokea haya usipokuwa makini:
- Kuumwa kichwa au kizunguzungu baada ya zoezi.
- Kusinzia kupita kiasi.
- Kutengeneza Kumbukumbu ya Uongo (False Memories) – yaani unaweza kuingiza kumbukumbu ya tukio ambalo hujawahi kulifanya na ukaamini ni kweli.
Onyo: Hypnosis haitakiwi kufanywa kwa watu ambao hawako sawa kiakili (wagonjwa wa akili). Kufanya hivyo ni sawa na kuzima moto kwa kutumia petroli.
Jinsi ya Kufanya Self-Hypnosis (Mwenyewe)
Ili kujifanyia Hypnosis wewe mwenyewe kwa usalama, vaa nguo zinazokufanya ujisikie huru (comfortable) kisha fuata hatua hizi:
Hitimisho
Usijilazimishe kufanya mambo ambayo ni kinyume na asili au imani yako. Tumia uwezo huu wa kiakili kujiponya wewe na wenzio dhidi ya hofu, misongo ya mawazo, na tabia zinazokurudisha nyuma.