Njia ya kuvuta Pesa kwa kutumia Jani La Bay

Rakims Spiritual
0

Njia ya kuvuta Pesa kwa kutumia Jani La Bay

Awali ya yote fahamu ya kuwa hii ni njia ya kale kiasi hivyo kwa wakati uliyopo hakikisha watu wa sasa hawakuoni nayo kwa maana watu wa sasa wana mambo mengi ya hovyo;

Elewa ya kuwa maada husika au wahusika hapa ni wasimamizi wa moto au watumishi wa maada ya moto.

Nayo hii ni moja ya njia ambazo kwa mtu mwenye kutaka pesa haraka haraka ana dharula basi ndio inamfaa zaidi.

Majani ya Bay yalikuwa yakitumika kwa njia nyingi za kitakatifu kipindi cha wagiriki zama za kale, na yanafahamika sana na waroma kwa nafasi kubwa ya kuwawezesha kutimiza mahitaji yao kwa njia za haraka za kustaajabisha.

Faida zake zingine ni pamoja na;

1. Kinga
2. Kufungua vifungo
3. Mvuto wa pesa
4. Dhamira ya dhati na haraka kwa matokeo

Kwa upande wa Pesa za Moto

Tutaanza kama ifuatavyo:

1. Maandalizi: Chukua majani mawili ya Bay ambayo ni makavu sana na ukavu wake uwe ni wa asili ya kuunguzwa na jua hadi likadondoka lenyewe chini. Kama ni pesa kiasi na huna kazi utatumia kwa kupata pesa kama zali basi utatumia maka pen ya Kijani.
Kama una biashara na unataka kuongeza pesa za mtaji basi wewe inakufaa zaidi makapeni ya Rangi ya Dhahabu au Machungwa.

Hakikisha unaandika katika jani hilo aya hii kwa kihebrania au kiarabu; "Yeye ndiye anayefisha vilivyo hai na kuwa wafu na yeye ndiye anaefufua wafu na kuwa hai Mwingi wa Rehema mwenye Kuruzuku."

Kuandika kiarabu;

هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ

Kuandika Kihebrania

הוּא אֲשֶׁר מֵמִית אֶת הַחַיִּים וּמְחַיֶּה אֶת הַמֵּתִים, רְחַב הָרַחֲמִים, הַמְפַרְנֵס.

Au kwa kiswahili chako;

Hu asher memit et ha'chayim u'me'chayeh et ha'metim, re'chav ha'rachamim, ha'mefarnes.
Kisha chini kiasi au nyuma utaandika kiasi cha pesa unachohitaji na kwa muda unaohitaji. Na kwa wale wenye biashara wataandika kiasi cha ongezeko la mapato.

2. Kujaza Jani Hili: Shikilia jani hilo kwa mikono miwili kwa kuifumba kama vile wanavyofanya wakristo wakiwa wanafanya ibada, Yaani mikono ya Shukran.
Kisha fumba macho yako na ujijenge katika fikra zako namna au katika hali utakayopokea ruzuku yako, Hakikisha picha yako na hisia zako zimehisi kabisa kuwa teyari hiyo pesa unayo.

3. Kuachilia: Ili kuweza kuachilia nguvu hiyo basi hakikisha kuwa haiitwi nguvu isipokuwa baada ya kukuvaa lazima uachilie, Ili kusudi isije kufunga zingine baadae, Kwa aliyetumia maker pen ya kijani basi ahakikishe ametumia na mshumaa wa kijani.

Na aliyetumia marker pen ya Dhahabu basi atumie mshumaa mweupe. Utatoa majani yako mawili ambayo moja la kushoto na lingine la kulia.
Kwa mwenye kuita pesa atumie mkono wa kushoto ndio achome na mwenye kuongeza atumie mkono wa kulia vile ulivyokuwa umeyafumba. 

Chukua tweezer au kibanio kisha usogeze kwenye moto wa mshumaa.


4. Hatua ya mwisho: Kama vile moshi unavyopaa kwenda juu basi ndivyo hivyo hivyo weka akilini (Manifestation) kuwa kama linavyoenda na moshi huu ndio litafute ulimwenguni hitaji langu litimie kwa muda wangu.

Pata majivu yake na yaweke juu ya Jani la pili kisha toka nayo nje angalia upepo unaelekea wapi na kama hamna upepo, Puliza kuelekea kaskazini kama unatafuta pesa, na puliza kwenda mashariki kama unatafuta wateja/kuongeza mtaji.




Njia ya kuvuta Pesa kwa kutumia Jani la Bey

Onyo/Ukumbusho.

Hakikisha unarejesha nguvu hii kwa kurudisha Bakh Bakh bi Haqq Bakh bi Salaam.
Barakallahu fii kum.

Hususani kwa watu wote wenye nyota zinazogawanyika kwa 2.

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)
Our website uses cookies to enhance your experience. Learn more
Accept
💬 Get Guidance